Pande mbili zinazohasimiana na
kusababisha kuzuka upya kwa vurugu nchini Sudan Kusini zimetangaza
kusitishwa kwa mapigano,baada ya kuwepo kwa siku kaadhaa za machafuko
mjini Juba zilizosababisha vifo vya mamia ya watu.
Mapigano baina
ya majeshi yanayomtii Rais Salva Kiir na yale yanayoongozwa na Makamu wa
Rais wa kwanza Riek Machar yanatishia kuharibu mkataba wa amani
uliosainiwa mwaka jana kumaliza miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa
wenyewe.Machar ameiambia BBC machafuko ya hivi karibuni yamesababishwa na watu wasiotaka kuona amani ikiwepo nchini humo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametoa wito wa kuimarishwakwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusin



No comments:
Post a Comment