Jeshi
la Polisi limekwama kuwafikisha mahakamani viongozi wanne wa Taifa wa
Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya kukosea hati ya
mashtaka.
Wanaoshikiliwa
ni Mwenyekiti wa Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita,
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa Mkoa wa
Mbeya, George Tito.
Akizungumza
jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema makosa
yametokea wakati wa uandaaji wa hati ya mashtaka.
“Mahojiano
yameisha, charge sheet (hati ya mashtaka) ikaandaliwa, lakini
ikarudishwa tuifanyie marekebisho. Muda umepita wa Mahakama watapelekwa
kesho (leo),” alisema.
Hata
hivyo, alisema kesi hiyo haina dhamana kwa upande wa kituo cha polisi
na hivyo kuwalazimu watuhumiwa hao kuendelea kukaa rumande.
“Wasubiri kesho (leo) wataka- poenda mahakamani kama wataamua kuwapa dhamana,” alisema Mambosasa.
Kuhusu
baadhi ya watuhumiwa hao kugawanywa katika selo tofauti za Chamwino na
wengine kuachwa Kituo Kikuu cha Polisi, Mambosasa alisema huo ni
utaratibu wa kawaida ambao unalenga kupata maelezo ya kila mmoja.
“Hayo
ni mahojiano tu ili kila mmoja upate anasema nini ndipo unawaweka
sehemu tofauti. Hizo ni taratibu za mahojiano ili wasiendelee na
mawasiliano,” alisema.
Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi alisema kisheria watuhumiwa hawatakiwi kukaa rumande kwa zaidi ya saa 24.
“Cha
kusikitisha siku ya leo (jana) ambayo walisema wangewaleta mahakamani
kwa kile wanachoamini wametenda kosa, lakini hadi sasa muda wa mahakama
unaisha viongozi wetu hawajaletwa,”alisema na kuongeza:
“Na
sisi tunataka kuondoka ili tuone taratibu nyingine ambazo zinaweza
kutuhakikishia usalama wa viongozi wetu. Hadi sasa viongozi wetu
hawajaletwa mahakamani.”
Alisema
hata kama polisi wanawaona viongozi wao wanamakosa, kisheria hawawezi
kukaa na mtu kwa muda wa siku tatu bila kumfikisha mahakamani.
Alisema
utendaji wa polisi nchini ni tofauti na wa nje ya nchi ambapo kwa nchi
za wengine, polisi ni sehemu ya huduma na si ya mabavu.
Alisema hali hiyo inaleta kadhia na masumbuko kwa Watanzania na hivyo kupunguza imani yao kwa jeshi hilo.
Wakili
wa watuhumiwa hao, Fred Kalonga alisema wamekuwa na wateja wao tangu
siku walipokamatwa kwa kuhakikisha wanahojiwa kwa mujibu wa sheria.
“Kwa
mujibu wa ahadi za polisi kuwa leo (jana) wanaletwa mahakamani. Kuanzia
saa 1.30 asubuhi tuko mahakamani na sasa inakwenda saa 9.30 alasiri
hakuna mtuhumiwa aliyeletwa. Kimsingi muda wa mahakama umeisha,” alisema.
Alisema
yeye na wakili mwenzake, Azack Mwaipopo walikuwa wanakwenda kufuatilia
taratibu nyingine za kisheria za kuwawezesha kupata dhamana.
“Tunakwenda
kufuatilia taratibu nyingine lakini sisi tupo tayari muda wowote
wakiletwa tutawadefend (tutawatetea) kwasababu tunaamini kwa mujibu wa
maelezo ya wateja wetu wapo sahihi kuliko tuhuma zinazowakabili,” alisema.
Wanachama
wa Chadema walikuwa katika viwanja vya mahakama tangu saa 2.00 asubuhi
hadi saa 9.30 alasiri baada ya kuelezwa na wakili wa watuhumiwa kuwa
viongozi wa Bavicha hawatapelekwa mahakamani tena.
Viongozi
hao walikamatwa Ijumaa usiku katika baa ya Capetown walipokwenda kunywa
na kula chakula. Wanadaiwa kwa tuhuma za kukusudia kuikashfu Serikali.
Akizungumzia
mpango wa vijana wa Chadema kuzuia mkutano wa CCM utakaofanyika Julai
23 mjini hapa, Sosopi alisema wanaiheshimu kauli ya Mwenyekiti wa Chama
hicho, Freeman Mbowe ya kuwataka kutokwenda kuzuia mkutano huo.
“Tunaiheshimu
kauli ya mwenyekiti na tunatambua kuwa vijana wengi nchi nzima
wamejiandaa kwenda kuzuia mkusanyiko huo, lakini sasa tunashughulika na
hili la viongozi wetu kukamatwa kwanza,”alisema.
Alisema
baada ya viongozi wao kupata dhamana wataitisha kikao cha Kamati ya
Utendaji ya Bavicha haraka ili kujadili suala hilo na watatoa msimamo
kama wanakuja na mkakati mwingine ama kuendelea na huohuo.
|
July 12, 2016
VIJANA WA CHADEMA WATII AGIZO LA MBOWE...VIONGOZI WAO KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment