![]() |
Meneja
Mradi anayesimamia upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma kutoka Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mbila Mdemu (wa kwanza
kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (wa pili katikati) kuhusu maendeleo yaliyofikiwa
katika upanuzi wa uwanja huo mkoani Dodoma.
“Kasi
ya ujenzi wa uwanja huu unaendelea vizuri kwa kushirikiana na
mkandarasi wa kampuni ya Chico na kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa
wakati kwa kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa”, amesema Eng. Mbila.
Upanuzi
wa uwanja wa ndege wa Dodoma unahusisha njia ya kuruka na kutua kwa
ndege yenye urefu wa Km 2.5 na mita 500 za taa za kuongozea ndege na
usalama wa kuruka kwa ndege .
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
|
![]() |
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja Mradi anayesimamia upanuzi wa uwanja
wa ndege wa Dodoma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Eng. Mbila Mdemu (wa tatu kulia) wakati alipokagua maendeleo ya upanuzi
huo.
Kuhusu
suala la kufufua ATCL Waziri Mbarawa amesema kuwa Serikali imeshalipa
kiasi cha sh. Bilion 36 sawa na asilimia 40 katika hatua za ununuzi wa
ndege mbili.
“Kama
ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano tutahakikisha hatua za
ununuzi wa ndege mpya zinafanyika kwa haraka ili kuweza kulifufua
shirika letu la ndege na kuweza kuanza kutoa huduma za usafiri wa anga
ifikapo mwezi septemba mwaka huu”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Kwa
upande wake Meneja Mradi wa upanuzi wa uwanja huo kutoka Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mbila Mdemu amesema kuwa mpaka
sasa mita 900 imekamilika kwa kuweka tabaka la kwanza lami katika eneo
la kuruka na kutua ndege na kazi ya kuchimba na kusawazisha eneo la
kurefusha njia imekamilika.
|
![]() |
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameridhishwa
na maendeleo ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo mpaka sasa
ujenzi huo umefikia asilimia 35 ikiwa ni kazi iliyotekelezwa ndani ya
siku 18 toka alipotoa agizo hilo mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.
Ametoa
kauli hiyo alipokuwa akikagua ujenzi wa uwanja huo na kumhimiza
mkandarasi wa Kampuni ya Chico kuendeleza kasi ya ujenzi huo ili
kukamilisha kwa wakati uliopangwa na kutoa msisitizo kwa makandarasi
wengine wanaotekeleza miradi mbalimbali nchini kujipanga na kufanya kazi
kwa ushirikiano ili kukamilisha miradi hiyo kwa muda mfupi kulingana na
makubaliano ya mikataba.
“Mradi
huu umetupa mfano kama tukijipanga vizuri hata kwenye miradi mingine
tunaweza kutekeleza kwa haraka na ubora unaotakiwa, kwa upande wetu kama
Serikali tutahakikisha uwanja huu unakamilika haraka ili kuruhusu ndege
kubwa kuanza kutua”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Aidha
ameongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa chachu kwa
Shirika la Ndege Tanzania ATCL kuwaunganisha watanzania kwa kutoa
huduma za usafiri anga katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo
kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
|





No comments:
Post a Comment