![]() |
Wapinzani
wengine wa Young Africans, katika michuano ya kuwania Kombe la
Shirikisho Barani Afrika, timu ya mpira wa miguu ya Medeama kutoka
Ghana, itawasili Dar es Salaam, Tanzania Alhamisi Julai 14, 2016 kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ), imefahamika.
Young
Africans itaikaribisha Medeama ikiwa ni mchezo wa tatu kuwania taji
hilo hatua ya makundi. Mchezo utafanyika saa 10.00 jioni Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam Julai 16, mwaka huu.
Huu
ni mchezo wa tatu kwa Young Africans katika harakati za kuwania Kombe
la shirikisho hatua ya makundi. Michezo miwili ya awali ilikuwa ni dhidi
ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza
tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Mchezo
wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour
El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir
Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid
Mansour.
Kamishna
wa mchezo huo atakuwa Pasipononga Liwewe kutoka Zambia na maofisa
wasimamizi ni Mfubusa Bernard ambaye atasimamia utendaji wa waamuzi
wakati Mratibu Mkuu wa mchezo huo kutoka CAF atakuwa Ian Peter Keith Mc
Leod.
Kikosi cha Yanga KIkosi cha Medeama |
July 13, 2016
WAPINZANI WA YANGA KLABU YA MEDEAMA KUTUA KESHO ALHAMISI JULAI 14 DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





No comments:
Post a Comment