![]() |
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeongeza muda zaidi kuimarisha
idara zake ambako imeongeza muda wa wiki moja kwa Watanzania wenye sifa
za Idara ya Masoko na Habari ili kuongoza Idara hiyo.
Awali
tarehe ya mwisho ilikuwa Julai 11, 2016 lakini kwa sasa tarehe ya
mwisho itakuwa Julai 19, mwaka huu kwa nafasi ambazo TFF imetangaza
ajira.
Lengo
hasa ni kuendana na hali halisi ya uendeshaji mpira wa miguu duniani
ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za
kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu
popote duniani.
Pili
ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpira wa miguu zinatokana na
soka na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati
mwafaka.
Kwa nafasi za kazi TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz
Mbali
ya kuboreshwa kwa Idara hiyo ya Masoko, pia TFF imepania kutoa
kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha madawati
ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi. Hapo awali madawati ya wanawake na
waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea (Volunteers) au wa muda
(Part timers).
Akizungumza na www.tff.or.tz,
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali
za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji
vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za
wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka la wanawake.
Kuhusu
waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto nyingi
hasa hasa katika kupata waamuzi wenye viwango vya Kimataifa.
|
July 13, 2016
TFF YAENDELEA KUSAKA NAFASI YA MKURUGENZI WA MASOKO,WENYE SIFA WAOMBWA KUJITOKEZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment