KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 30, 2016

DALADALA LAGONGA MAGARI MATATU MAJI MATITU TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI

DAL
 Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.
 Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
 Daladala hiloegonga gari namba T 458 CAN.
 Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
 Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.
 
Na Dotto Mwaibale
 
MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia.
 
Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo  asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi.
 
Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.
 
” Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro” alisema Juma.
 
Alisema baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.
 
Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.
 
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.
 
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa simu mara kadhaa.
 

No comments:

Post a Comment