![]() |
Katika siku za hivi karibuni,
kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine
mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na
usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za
kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria,
kanuni na taratibu za Nchi.
Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za
makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo yake ya mwaka 2002, kifungu cha
178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya
ulinzi na usalama, kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu
yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi
yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo bila kibali
kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia kitendo kilichofanywa na
kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na
sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam
linachukua hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.
Aidha Jeshi la Polisi nchini,
linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi
yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama hapa
nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria
dhidi yake.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa
wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na
usalama kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu
nao.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
|
August 16, 2016
MATUMIZI MABAYA YA SARE ZA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment