KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 16, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWAJULIA HALI SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI PAMOJA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN SAMUEL MALECELA JIJINI DAR ES SALAAM.

MAG3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.
MAG6
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Spika Sala sala jijini Dar es Salaam.
MAG7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.
MAG8
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.
MAG9
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango Malecela.
MAG10
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai wakati alipokwenda na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.
MAG11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.
MAGU4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali.

No comments:

Post a Comment