
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akitoa
maelekezo ya namna ya kutumia mfumo wa tiketi za eletroniki kwa Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa
akikagua vifaa vya mfumo huo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es
Salaam Agosti 22,2016.

Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa
Bw. Julius Mgaya(katikati) akimuonesha moja ya mashine ya tiketi za
kieletroniki Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam Agosti 22,2016.

Eneo lililowekwa mageti kwa ajili ya mashine za mfumo wa tiketi za eletroniki katika Uwanja wa Taifa.
Picha na Genofeva Matemu – WHUSM
……………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Serikali inatarajia kuongeza
mapato katika Uwanja wa Taifa kwa kutumia mfumo wa tiketi za elektroniki
ambapo wateja watahitajika kuwa na kadi za e-wallet pamoja na kufanya
malipo kwa njia ya mtandao ili kuingia uwanjani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua
akikagua vifaa vya mfumo huo leo jijini Dar es Salaam katika uwanja wa
Taifa.
Mhe. Nnauye amesema kuwa Mfumo wa
elektroniki unatumia umeme na una UPS inayohifadhi umeme kwa masaa
matatu hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusiana na mfumo huo kwani
unatarajiwa kukidhi huduma kwa wananchi wote watakaotumia uwanja wa
taifa katika matukio mbalimbali.
“Ni vema wananchi mkajenga
utamaduni wa kuwahi uwanjani wakati wa mechi ili kurahisisha na kutumia
kwa makini mfumo wa elektroniki katika uwanja wa taifa unaotarajiwa
kakabidhiwa rasmi tarehe 4 Septemba mwaka huu kwa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo” alisema Mhe. Nnauye


No comments:
Post a Comment