
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
……………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali inatarajia kutatangaza
zabuni kwa ajili ya kupata kampuni itayojenga kijiji cha michezo
changamani kilichopo Temeke Jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye wakati akipokea uwanja wa Uhuru kutoka kwa kampuni ya CBG
baada ya kufanyiwa matengenezo.
Mhe. Nape Moses Nnauye amesema
kuwa azma ya kujenga kijiji cha changamani ni ya muda mrefu na kuna
mchakato wa kutengeneza ubia kati ya Serikali na wadau wengine wa
michezo ili kutekeleza mradi huo.
“ Tutatangaza zabuni kwa makampuni
ili waweze kutuma maombi yao kwa ajili ya kutekeleza mradi huu na
tutapitia kwa kina na umakini maombi yote ili kupata mtu sahihi”
alisema Mhe. Nape.
Mhe. Nape Moses Nnauye ameongeza
kuwa Serikali tayari imeshaandaa eneo na ramani kwa ajili ya ujenzi
na hivyo kuwapa nafasi wadau watakaopenda kujenga mradi huo.
Amesisitiza kuwa mchakato huo sio
wa siku moja kwa kuwa kuna taratibu za kisheria zinahitajika kufuatwa
ili kutekeleza mradi huo katika viwango vya kimataifa.
Eneo changamani ni eneo la kwa
ajili ya ujenzi viwanja vingi vya michezo vitakavyotumika katika kukuza
na kuinua vipaji vya michezo nchini


No comments:
Post a Comment