KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 28, 2016

MADEREVA GEITA WAPIMA AFYA ZAO

zac01
Viongozi wa serikali na Jeshi la polisi wakipata maelezo jinsi  huduma zinavyotolewa katika Zahanati Mwendo
zac2
Viongozi wa serikali na Jeshi la polisi wakipata maelezo jinsi  huduma zinavyotolewa katika Zahanati Mwendo
zac3
Madereva wakipima afya zao
zac4 
Mwonekano wa Zahanati Mwendo kwa nje
……………………………………………………………….
-Wananchi wapata mafunzo ya unywaji kistaarabu
Huduma ya Zahanati Mwendo ambayo imebuniwa na kampuni ya TBL Group katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani kwa ajili ya kupima afya za madereva imekuwa kivutio kikubwa mkoani Geita ambako maadhimisho haya yamezinduliwa kitaifa na idadi kubwa ya madereva na wananchi wanaendelea kujitokeza kupima afya zao kwa wingi na kupatiwa matibabu na ushauri nasaha.
Madaktari maalumu waliopo kwenye gari la kufanyia vipimo la Zahanati Mwendo muda wote tangia kuwasili mkoani Geita  wamekuwa na kazi  kubwa ya kutoa huduma kwa madereva wengi na wanaendelea kujitokeza kufanyiwa vipimo siku hadi siku.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group ,Amanda Walter,amesema  inavutia kuona watanzania wengi wanahitaji huduma ya kupimwa afya  na kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa madereva na wananchi wanaotembelea Zahanati Mwendo.
Alisema pia kuwa wananchi wengi wamejitokeza katika semina ya Mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu yaliyofanyika katika kituo Kikuu cha mabasi cha Geita ambapo walipata fursa ya kujua madhara ya matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kupindukia.
”Wiki ya Usalama ya mwaka huu imekuwa na mwamko mkubwa hususani wananchi walivyojitokeza kwa wingi katika mafunzo haya ya Unywaji wa Kistaarabu na mengine yanayohusina na Usalama barabarani.TBL Group tunaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kampeni za Usalama kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali nchini”Alisema.
Rehema Nyoki,mkazi wa Geita ambaye amehudhuria mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu akiongea kwa niaba ya wenzake aliipongeza kampuni ya TBL Group kwa kuendesha semina za uhamasishaji unywaji kistaarabu  na alitoa ombi  mafunzo hayo yafikishwe sehemu mbalimbali nchini kwa kuwa ipo idadi ya waathirika wengi wa kutumia vinywaji vyenye kilevi kupita kiasi  kwenye jamii ambao wanaishia kupata matatizo ya kila aina.

No comments:

Post a Comment