Mgogoro
ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado unafukuta ambapo jana Prof.
Ibrahim Lipumba, aligomea mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la chama
hicho ulioitishwa leo visiwani Zanzibar
Alisema,
taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari kuhusu kufanyika kwa mkutano
huo hazitambui kwa kuwa, mamlaka zinazohusika kuitisha kikao hicho
hazijakidhi matakwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini
Dar es Salaam kupitia taarifa iliyoandaliwa na Magdalena Sakaya, Naibu
Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa na chama hicho alisema, matakwa ya
katiba hayakuzingatiwa.
“Wajibu
wa Kamati ya Utendaji ya Taifa utakuwa kuandaa.. agenda za Baraza Kuu
la Uongozi la Taifa na kutayarisha na kuhifadhi mihtusari ya vikao vyote
vya Mkutano Mkuu wa Taifa, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na vya kamati
ya utendaji ya taifa yenyewe na kuwasilisha taarifa ya yatokanayo
kutokana na utekelezaji wa maamuzi ya kikao kilichohusika kilichopita,” Prof. Lipumba amenukuu katiba ya chama hicho ibara ya 85(5).
Prof.
Lipumba alisema, Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho
yupo nje ya nchi na kwamba, kutokana na Katiba ya CUF,Naibu
Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu Mkuu kwa madaraka ni yule aliyetoka
upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka Katibu Mkuu
Kwa upande wake Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa alisema;
"Mimi
sijaitisha wala sina taarifa ya kikao cha kamati ya utendaji
kilichofanyika Zanzibar, kwa taarifa nilizonazo hakuna wajumbe wa kamati
ya utendaji kutoka Bara waliokua Zanzibar wakati wa kikao hicho.
Nachukua nafasi kuwajulisha wajumbe wote wa baraza kuu kuwa hakuna kikao
chochote cha baraza kuu kilichoandaliwa na kamati ya utendaji ya Taifa
ambayo kikatiba mimi ndiye mwenyekiti wake wakati katibu mkuu hayupo.
“Mimi
ndiye mwenye mamlaka ya Katibu Mkuu kwa sababu Naibu Katibu Mkuu wa CUF
Tanzania Bara kikatiba ndiye msimamizi namba moja wa Katibu Mkuu” .
Alisema, Katiba ya CUF ya mwaka 1992 Toleo la 2014 kifungu cha 95 (3) kinaeleza “Naibu
Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu Mkuu kwa madaraka ni yule aliyetoka
upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka Katibu Mkuu,” na kwamba, Katibu Mkuu anatoka Zanzibar na yeye anatoka Bara.
Hata hivyo Prof. alisisitiza kuwa, Sakaya hana taarifa ya kikao hicho cha kamati tendaji kilichofanyika Zanzibar.
Pamoja
na kuwepo kwa sintofahamu kutokana na uamuzi wa Jaji Mutungi kumtambua
Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho, (Lipumba)
amepongeza kurejeshwa kwake.
Prof.
Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho aliyesimamishwa na CUF mwezi
uliopita, alirejea kwenye nafasi hiyo kwa kauli ya Jaji Mutungu, Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini.
Prof.
Lipumba alieleza kushangazwa na hatua ya Jaji Mutungi kukosolewa na
baadhi ya wanasheria na majaji mashuhuri kuwa, hakuna sheria inayompa
furasa jaji huyo kuchukua hatua aliyoichukua.
No comments:
Post a Comment