| Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya wakitoa burudani katika hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu matano ambavyo vimejengwa kwa msaada wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 8. |
| Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ipinda Subira Gwakabale akishukuru kwa kupatiwa msaada na benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kujengewa vyoo vya walimu vyenye matundu 5 kwa thamani ya shilingi milioni 8 ,ambapo pia katika katika shukrani zake ameelezea changamoto mbalimbali walizonazo ikiwa ni pamoja na Idadi kubwa ya wananfunzi kuliko vyumba vya madarasa walivyo navyo ambapo kwa sasa wana jumla ya wanafunzi 948 huku vyumba vya vya madarasa vikiwa 8 tu hali ambayo inawawia vigumu katika utoaji wa huduma kwa wanafunzi hao. |
| Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya ,Humphrey Julias akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu matano ambavyo vimejengwa na benki hiyo katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela. |


No comments:
Post a Comment