
Na: Mwandishi wetu
Bodi ya Filamu Tanzania leo
imemkabidhi cheti na hundi yenye thamani ya shilingi Laki Mbili
mwanafunzi Omary Maganga aliyefanya vizuri kwenye masomo ya filamu na
runinga kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA).
Makabidhiano hayo yamefanyika
kwenye ofisi za bodi hiyo ambapo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Abuu
Kimario alimkabidhi cheti hicho na hundi kwa niaba ya Katibu Mtendaji
Joyce fisoo.
Baada ya kukabidhiwa zawadi
zake bwana Maganga aliishukuru Bodi hiyo ya filamu kwa kutambua juhudi
za wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao. Pia ameziasa taasisi
zingine za Serikali na zisizo za kiserikali kuwatambua wanafunzi
wanaofanya vizuri kwani kwa kufanya hivyo kunaongeza morali na
ushindani.
Wakati huo Afisa Uhusiano na
Mawasiliano Abuu Kimario kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa bodi hiyo
ametoa ahadi ya kuendelea kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri
kwenye masomo yenye uhusiano na tasnia ya filamu.
Kwa sasa Bodi ya Filamu Tanzania
iko kwenye utekelezaji wa programu ya kutambua na kukuza vipaji vya
wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya tasnia ya filamu nchini.
Program hii ilianzishwa ikiwa na lengo la kukuza ubora wa filamu za
Kitanzania


No comments:
Post a Comment