
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa
Congo (DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (kulia) akisisitiza jambo
kwa waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa wafanyabiashara wa Congo
kutumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya Serikali kuondoa vikwazo,
kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bw. Tiganya Vincent.

Baadhi ya waandishi wa habari
wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo (DRC)
nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (mwenye suti) wakati alipokuwa
akielezea kuridhika na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kuondoa vikwazo
katika Bandari ya Dar es Salaam na kupelekea wafanyabiashara wa Congo
(DRC) kuendelea kuitumia bandari hiyo.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
Na: Frank Shija, MAELEZO.
WAFANYABIASHARA kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo wafurahishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali
ya Tanzania katika kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa mizigo kupitia
Bandari ya Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Rais wa
Wafanyabiashara wa Congo waishio nchini Tanzania Bw. Sumaili K. Edward
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kurejea kwao na
kutumia Bandari hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Sumaili amesema kuwa miaka ya
nyuma kulikuwa na changamoto nyingi ambapo alizitaja kuwa ni mizani na
sehemu za ukaguzi kuwa nyingi pamoja na siku za kuhifadhi mizigo kuwa
chache.
Alisema kuwa wamefikia uamuzi wa
kuendelea kutumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya Serikali ya Awamu ya
Tano kutatua changamo hizo ambapo sasa vizuizi vimepungua.
“Naipongeza Serikali ya Tanzania
kwa hatua ya kutuondolea usumbufu sisi wafanyabiashara wa Congo
tuliokuwa tunafanya shughuli zao Bandari ya Dar es Salaam, tumerejea na
tutapitishia mizigo yetu hapa”. Alisema Sumaili.
Adhai alisema kuwa wamefarijika
kuona sasa siku za kuhifadhi mizigo kabla ya kuongezeka kutoka siku 15
zilizokuwepo awali hadi kufikia 30 kama ilivyobainishwa wakati wa ziara
ya siku tatu ya Rais wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
mapema wiki hii.
Akijibu swali la la mwandishi wa
habari aliyetaka kujua sababu zilizowafanya kusitisha kwa muda kutumia
Bandari ya Dar es Salaam, Rais huyo alisema kuwa kitu kikubwa kilicho
wafanya wachukue uamuzi wa kusitisha ni gharama kuwa kubwa hivyo
kupelekea kufanya biashara isiyokuwa na faida.


No comments:
Post a Comment