KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 12, 2016

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAFANYA KONGAMANO LA MIIKO YA UONGOZI

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinatarajia kufanya kongamano maalum la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere 14 Oktoba,2016 huku Mada Kuu ikiwa ni:  Miiko ya  Uongozi na Azimio la Arusha.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam mapema leo 12 Oktoba,2016 Mkuuu wa Chuo hicho, Profesa. Shadrack Mwakalila ameinisha kuwa kongamano hilo ni maalum katika kumuenzi Mwalimu Nyerere tokea kifo chake kilichotokea miaka 17 iliyopita.
“Lengo ni kumuenzi kwa viendo. Hivyo watu mbalimbali wageni waalikwa na watoa mada wataelezea namna ya Miiko ya uongozi na namna Azimio la Arusha.
Mada juu ya Azimio la Arusha itatolewa na Dkt. Harun Kondo huku Mada ya Miiko ya Uongozi itatolewa na Mh.Wilson Mkama, Mh. Joseph Butiku. Pia wapo Mh. Ibrahimu Kaduma na  Mh. Phillip Mangula” amesema Mkuu wa chuo huyo, Profsa Mwakalila.
Aidha, amesema kuwa, tukio hilo litafanyika chuoni hapo katika ukumbi wa Utamaduni ambapo viongozi mbalimbali wa Kiserikali, binafsi na wananchi wengine wanaalikwa na ni bure ilikuweza kujifunza namna ya falsa za Baba wa Taifa katika misingi imara ya maadili ya kazi na utawala

No comments:

Post a Comment