MTOTO
wa kike anayekisiwa kuwa na umri kati ya miezi minane na mwaka mmoja
amefikishwa katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete na wasamaria
wema baada ya kutekelezwa na mama yake mzazi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya
Wete , Amina Ali Mabrouk mkaazi wa Bopwe Jimbo la Gando ambaye aliachiwa mtoto huyo na mama yake , alisema mama mzazi wa mtoto huyo alimtelekeza mwanawe siku ya Jumatatu jioni kwa madai anakwenda kutelekeza ibada ya sala ya jioni .
Alieleza
kwamba baada ya kukabidhiwa kichanga hicho , mama mzazi hakutokea tena
ambapo alichukua hatua za kwenda kuripoti kituo cha polisi Wete kwa
hatua za kisheria kwa kuwa mtoto huyo alikuwa anahitaji huduma .
“Nilikuwa
katika biashara zangu kigengeni , mara alitoa mama mmoja hanijui wala
na mimi simjui , alinitaka nimsaidie mtoto ili aende kutekeleza ibada ya
sala lakini kuanzia muda huo sikumuona tena ”alieleza.
Aidha
aliongeza kwamba “Ilipofika saa nne usiku ilinibidi niende kutoa
taarifa kwa sheha na baadaye Polisi ambapo nilitakiwa nimfike leo (jana)
asubuhi , nimefika mapema nikaambiwa nije ofisi ya Ustawi wa jamii ”aliongeza.
Afisa
Ustawi wa Jamii Wilaya hiyo Salma Suleiman amekiri kupokea kichanga
hicho na kusema hatua ya kwanza ni kumpeleka hospitali kwa ajili ya
uchunguzi wa afya yake huku hatua nyingine zikiendelea kuchukuliwa .
Alisema
katika kuhakikisha mama mzazi anapatikana , Ofisi ya ustawi wa jamii
imeanza kuwasiliana na viongozi wa shehia ili kusaidia kupatikana mama
yake ambapo kwa sasa ataendelea kuhifadhiwa na Ofisi ya Ustawi wa jamii.
“Jambo
la kwanza ambalo Ofisi ya Ustawi itafanya ni kumpeleka Hospitali
kufanyiwa uchunguzi w afya mtoto huyo , halafu masuala mengine ya
kumtafuta mama mzazi zitafuatia baadaye ”alieleza.


No comments:
Post a Comment