Ali Issa na Mwanaisha Mohamed Maelezo Zanzibar
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Baloz
Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi dkt Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar itaendelea kutoa elimu bila malipo na Afya kwa wananchi wake
hapa visiwani.
Hayo ameyasema leo huko chuo cha
Afya Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar wakati alipokuwa katika
Mahafali ya Pili na ya 23 ya Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya madaktari.
Amesema Serikali inatambua
umuhimu wa elimu na Afya kwani ndio njia mojawapo ya kuleta
maendeleo,hivyo haina budi kuitoa huduma hiyo bila malipo kwanindio njia
maojapo yakuleta maendeleo katika nchi .
Aidha alifahamisha kua chuo cha
Sayansi ya taaluma ya Afya kwa sasa hakitakua tena chini ya usimamizi wa
Wizara ya Afya bali kitakua kipochini ya uangalizi wa SUZA.
Alisema kupelekwa huko ni kupata frusa nyingi pamoja na soko la ajira kutanuka.
Dkt. Shein alisema kuwa muajiriwa
yoyote katika utumishi wa umma atalazimika kufanya kazi popote ndani ya
nchihii kama alivyo tia saini makataba na hatasubutu kukataa sehemu
alio pangiwa kufanyakazi.
Nae Waziri wa Afya Mahamuod
Thabiti Kombo aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa uadilifu
wakizingatia lugha wanazo zitoa ziwe lugha tabibu ili mgonjwa aridhike
na matibabu na kupona haraka.
Alisema madaktari na wauguzi
watumie uzalendo wanapo wahudumia wagonjwa na kuthamini kazizao wao
wakiwa ni watu muhimu katika nchi.
Jumla ya wahitimu 525walitunukiwa
vyeti Chuoni hapo kwa kiwango cha stashahada ya uguzi,Afya na
Mazingira,Afisa Tabibu,Afya ya kinywa na Meno,Utabibu na Maabara na
madawa
No comments:
Post a Comment