Makame
Ali Makame Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polsi akisisitiza jambo kuhusu
matumizi mabaya ya simu za mikononi kwenye mkutano wa kuelimisha
wanafunzi wa skuli ya sekondari Kizimbani iliyoko mjini Wete kupinga
matendo ya udhalilishaji pamoja na njia bora ya kuwaheshimu walimu baada
ya kuibuka tabia ya kurushiwa chupa za mikojo walimu wawapo darasani na
baadhi ya wanafunzi wanaojiita manunda
Mmoja
wa Viongozi wa dini akizungumza na wanafunzi wa skuli ya Kizimbani
sekondari wilaya ya Wete juu ya kuibuka vitendo vya kurushiwa chupa za
mikojo walimu na wanafunzi wanapokuwa darasani .
Afisa kutoka Dawati la Jinsia
na Watoto kutoka jeshi la polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Juma
Salum akitoa elimu ya kupinga matendo ya udhalilishaji kwa wanafunzi wa
skuli ya sekondari Kizimbani wilaya ya Wete.
………………………………………………………………………..
Na Masanja Mabula –Pemba ..
JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba kupitia kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto limeanza kutekeleza mpango mkakati wa kukabiliana na matendo ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo wa ulawiti na utumiaji wa madawa za kulevya .
Katika
utekelezaji wa mkakati huo , watendaji wa jeshi la Polisi kitengo cha
Dawati la jinsia na watoto wameanza ziara ya kuzitembelea skuli za mjini
Wete na kuzungumza na wanafunzi , walimu pamoja na wazazi wa wanafunzi
walioacha masomo kutokana na sababu mbali mbali .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Mkuu wa dawati la Jinsia Jeshi la Polisi
Mkoani hapa Khamis Faki Simai alisema kwamba ziara hiyo pia zinatumika
kuwarejesha skuli wanafunzi walioacha masomo pamoja na wanaokaa nje ya
madarasa wakati wa masomo .
Amesema
uwamuzi wa kutekeleza mpango mkakati huo ni kutaka kupunguza matendo ya
udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo yale ya ulawiti na utumiaji wa dawa
za kulevya yanayowaathiri zaidi vijana waliochini ya umri wa miaka 18.
Alifahamisha
kwamba katika utekelezaji wa mpango mkakati huo , wameweza kupata
ushirikiano wa kutosha kutoka kwa walimu na wazazi wa wanafunzi ambao
wameahidi kutoa ushirikiano wao ambao wamekuwa wakiambana katika zoezi
la utoaji wa elimu kwa jamii .
“Mpango
mkakati ambao tumeanza kuutekeleza umelenga kutokomeza vitrndo vya
udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ya ulawiti pamoja na utumiaji wa dawa
za kulevya kwani tumelenga kuhakikisha kunakuweko na jamii yenye maadili
”alifahamisha.
Naye
Salama Juma kutoka kitengo cha dawati la Jinsia alisema jeshi la Polisi
linatambua umuhimu wa elimu katika kukuza uchumi wa nchi , hivyo
wameamua kuwarejesha wanafunzi skuli ili wakapate haki yao ya msingi .
Alisema
katika ziara na mikutano ambayo wameifanya imesaidia kuwarejesha baadhi
ya wanafunzi skuli waliokuwa wameacha skuli pamoja na kuwafanya
kuhudhuria masomo wanafunzi watoro .ambapo pia ameahidi kufanya
ufuatiliaji wao .
Mmoja
wa wazazi Ali Omar Kanchape amabaye mtoto wake alikuwa ni miongoni wa
waliokuwa wameacha skuli , alilishukuru jeshi la Polisi kuendesha mpango
mkakati huo ambao umesaidia kijana wake kurejea skuli .
Aliwataka
wazazi na walezi kuupokea kwa mtizamo chanya mpango huo na kuhakikisha
wanashiriki katika kuwaelimisha wanafunzi walioacha skuli pamoja na
watoto wa kupindukia kutambua faida ya elimu na hasara ya kuikosa kwake .
Kassim Thinei mwanafunzi wa kidato cha pili Skuli ya Mitiulaya ambaye
alikuwa ametoroka skuli ya kipindi kirefu aliwataka vijana wenzake
ambao wameacha skuli kurejea na kuendelea na masomo na kuachana na
makundi maovu ambayo hatma yake ni kujiingiza kwenye vitendo viovu .
Jeshi
la Polisi limeanza kutekeleza mpango mkakati huo , huku kukiwa na
taarifa mbaya za ongezeko la vijana wanajihusha na matendo ya ulawiti
katika Wilaya ya Wete
No comments:
Post a Comment