NA HERIETH SEMGAZA
Jeshi la Police Kanda Maalum Dar
es salam limesema matukio ya kiuhalifu jijini humo yameanza kupungua
hii ni kutokana na kutumia mbinu ya ulinzi shirikishi linaloundwa na
kiongozi wa serikali za mitaa kwa kusaidiana na police kadhaa,ili
kupunguza uhalifu.
Hayo yamesemwa na Kamishina wa
Police Kanda Maalumu ya Dares salaam Kamanda Simon Sirro mkutano na
waandishi wa habari kituo cha kati jijini Dar es salaam wakati
alipotaja idadi ya matukio yaliyojitokeza hivi karibuni jijini humo.
Kamanda Siro amesema jeshi hilo
limesikitishwa na uharibifu uliojitokeza siku ya tarehe 2 /10/2016
katika uwanja wa taifa ,nakueleza kuwa watafanya uchunguzi ili kubaini
watu wote walioshiriki katika uharibifu huo na kuwafikisha mahakamani
mara tu wanapokamatwa.
Kamanda Siro ameongeza kuwa
jeshi la police kanda maalumu ya Dar es salaam kupitia kikosi cha
usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali kuanzia tarehe
27/9/2016 hadi tarehe 2/10/2016 na kuingizia serikari kiasi cha jumla ya
tozo Tsh 464,790000/=
Pamoja na hayo amewaomba wananchi
kuwa wepesi kutoa taarifa za kiuhalifu bila woga pindi wanapoziona au
kusikia ili jeshi la polisi liendelee na kazi kubwa ya kudhibiti na
kutokomeza uhalifu jijini Dar es salaam.


No comments:
Post a Comment