
Mfaransa Jerome Dufourg
……………………………………………………………………………………
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Timu ya Yanga imeamua kwenda sawa na TP
Mazembe,Zamalek na Mamelodi kwa kumuajiri Mfaransa Jerome Dufourg kuwa
mtendaji mkuu wa klabu kwa kumpa mkataba wa miaka mitatu na anatarajia
kuja Dar kumalizana uongozi na kazi rasmi ataanza Novemba wanajangwani
wanasuka safu bora ya maendeleo ya klabu.
Mfaransa huyo aliyewahi kufanya kazi Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA)
na klabu ya FC Talanta ya Daraja la Pili Kenya anatarajiwa kuwasili Dar
es Salaam wakati wowote kuanza kazi na ataanza rasmi majukumu hayo
Novemba 19.
Mfaransa huyu mwenye umri wa miaka 30
atakuja Dar kumalizana na uongozi uliochini ya Mwenyekiti Manji na Yanga
ina malengo ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa hivyo
imeanza kusuka safu hatari na yenye uweredi na watu wenye mpira ndio
maana imemchukua Mfaransa huyu ambaye anaonekana ni mzoefu.
Jukumu la kwanza kubwa la Dufourg na kuhakikisha mapato ya klabu
yanazidi matumizi. Mwaka jana Yanga iliingiza Sh Bilioni 1.3 wakati
ilitumia Sh Bilioni 2.8.
Yanga ina mpango wa kubadilisha benchi
la ufundi lote mpaka sasa wameingia mkataba na kocha wa Zesco United ya
Zambia George Lwandamina aliyechukua mikoba ya Pluijm aliyejiuzulu
No comments:
Post a Comment