
Na Masanja Mabula -Pemba
SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar, imekabidhiwa rasmi Hospitali ya Abdalla Mzee
Mkoani, kutoka kwa Serikali ya Watu wa China baada ya Hospitali hiyo
kukamilika kwa Ujenzi wake.
Makabidhiano
hayo yaliyofanyika katika hospitali hiyo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa
Kusini Pemba, yakishuhudiwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar.
Akizungumza
na wananchi Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe:Mahmoud Thabit Kombo,
aliwataka wafanyakazi na wananchi kuithamini na kuitunza hospitali
hiyo, ili vifaa vilivyomo viweze kudumu kwa muda mrefu.
Alisema
hospitali hiyo ni hospitali ya wananchi wa Mkoani, Chake Chake, Wete,
Micheweni na Zanzibar kwa ujumla, hivyo jukumu la kulinda miundombinu
yake iko mikononi mwa wananchiwenyewe.
Kombo,
alisema kwa sasa Hospitali ya Abdalla Mzee ni Hospitali ya kisasa zaidi
kutokana na kuwemo kwa vifaa vya kisasa, pamoja na kuwa na hadhi ya
kuliko hospitali ya Mnazimoja iliyopo Unguja.
“Leo
Serikali ya watu wa China imetukabidhi hospitali hii, na
wametukabidhi ikiwa na vitu vingi na vipya vya kisasa zaidi, ambavyo
wagonjwa wataweza kutibiwa hapa hapa kuliko kwenda nje ya
Zanzibar”alisema.
Akizungumiza
juu ya madaktari, alisema tayari Serikali imeshaanza kulifanyika kazi
suala hilo, ili kuona huduma bora zinapatikana kutokana na uwepo wa
madaktari wa kutosha.
Waziri
Mahmoud, alisema Historia ya Zanzibar na China ni ya udugu, iliyoanza
tokea mwaka 1972 baada ya timu ya kwanza ya Madaktari wa kichina kufika
Zanzibar kuanza kujitolewa, hivyo ni vigumu udugu huo kuvunjika.
Hata
hivyo aliwatoa hofu wananchi wa Mkoani, juu ya Hospitali hiyo kuwa
wanaweza kuitumia na kuhamia ili Rais wa Zanzibar atakapokuja kuizundua
aweze kuona watu wanapatiw ahuduma hospitalini humo.
Kwa
upande wake Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Mhe:Xie Ziaowu,
alisema mradi wa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, ni moja ya kigezo cha
ushirikiano baina ya Zanzibar na China katika kujali maisha ya kijamii.
Alisema
kujengwa kwa hospitali hiyo ni miongoni mwa ziara iliyofanywa na
Mhe:Rais wa China Xi Jinping nchini Tanzania mwaka 2013 na kuonana na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed
Shein naviongozi mbalimbali mara mbili.
“China
inathamini sana urafiki na Ushirikiano uliopo baina ya Zanzibar na
Tanznaia na kutaka ushirikiano huo uweze kuendelea katika kukuza maisha
ya watu nchini”alisema.
Alisema
Madaktari wa Kichina waliopo Zanzibar, wataendelea kuwepo ili
kuhakikisha wanawahudumia wananchi wa Zanzibar katika utoaji wa huduma
muhimu kwa wananchi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Khamis Mussa Omar,
aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuendelea kushirikiana
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwani mashirikiano hayo ni ya muda
mrefu tokea mwaka 1964 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi leo.
Alisema
tokea wakati huo Zanzibar na China imeendelea kuwa na urafiki na
mashirikiano ya kudumu, ambapo china imesaidia Zanzibar mambo mengi
yakiwemo Uchumi kwenye viwanda, kilimo, Afya, Maji, Elimu na michezo kwa
upande wa Uwanja wa Mao.
Kwa
upande wa Miundombinu alisema, bado mradi mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa
Unguja jengo la abiria, ambalo linajengwa kwa sasa baada ya mashauriano
kufikiwa, ujenzi wa bandari kubwa ya Mpiga duri kwa mashirikiano na
China, pamoja na Mkonga wa mawasiliano.
“Tunategemea
mashirikiano haya yatazidi kuendelea baina ya Zanzibar na watu wa
Jamhuri ya China, tunawashukuru sana kwa msaada ambao wamekuwa
wakitupatia”alisema.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dr Juma Malik Akili, aliwataka wananchi wa Pemba
kuhakikisha wanavitunza na kuvithamini vifaa vilivyombo ndani ya
hospitali hiyo.
Alisema
vifaa hivyo vitasaidia kutambua maradhi na kutibu maradhi kwa kutumia
njia ya kisasa zaidi, hivyo ni jukumu la kila mtu kuhakikisha Hospitali
hiyo na hadhi yake inaendelea kudumu daima.
Naibu
waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe:Harusi Said Suleiman, alisema
tukio hilo ni la kihistoria kutokana na ukubwa wa hospitali hiyo, huku
akiwataka wananchi kuilinda miundombinu ya hospitali pamoja na vifaa.
Nae
,Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba, Bakari Ali Bakari aliiomba
Serikali kuruhusiwa kutumia jengo hilo kwa ajili ya kutoa huduma kwa
wananchi kwa sasa, pamoja na kupatiwa wafanyakazi wa kutosha kutokana na
ukubwa wa jengo wenyewe, na bajeti kuongezwa ili kuweza kulihudumia
jengo hilo.
Ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani ulianza mwaka 2014 na kujengwa na kampuni ya Jiangsu Provincial Construction Group Co. Ltd kutoka China.


No comments:
Post a Comment