![]() |
| Shirika
la Umeme nchini (Tanesco) limepewa miezi miwili kuhakikisha inafikisha
huduma ya umeme katika kiwanda cha kusindika matunda na kuzalisha juisi
na vinywaji baridi cha Bakhresa Food Products Ltd kilichopo Mwandege
wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.
Agizo
hilo limetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda hicho
iliyofanyika leo wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.
Amesema
kuwa ni ajabu kwa mwekezaji kuanza ujenzi hadi anamaliza na baadaye
anaanza uzalishaji halafu suala la nishati ya umeme linakuwa kikwazo
hali inayomlazimu mwekezaji kutumia nishati mbadala (Jenereta) kitu
kinachosababisha gharama za uendeshaji kuwa kubwa.
“Ninaagiza
hakikisheni mnafikisha umeme katika kiwanda hiki kabla ya mwezi wa 12,
nia ajabu sana mtu anaanza kujenga mnamuangalia tu, anamaliza
mnamuangalia, Meneja wa TANESCO upo? Hakikisha umeme unafika kama kuna
mtu ana kukwamisha niambie”. Alisema Rais Magufuli.
Aliongeza
ni imani yake kuwa baada ya umeme kufikishwa katika kiwaanda hicho
gharama za undeshaji zitapungua na kupelekea kufanya maboresho ya
maslahi ya wafanyakazi wake.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli ametumia wasaa huo kumuomba Mwenyekiti wa
Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa kuangalia uwezekano wa kufanya
uwekezaji kama huo katika maeneo mengine ya kikanda hili kutoa fursa
kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kupata soko la bidhaa zao.
Kwa
upande wake Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Makampuni ya Bakhresa
unasaidia kuchochea kilimo cha matunda na kutoa fursa ya soko la uhakika
kwa wakulima.
Mwijage
alisema kuwa Sekta ya Viwanda nchini imeendelea kukuwa, aliongeza kuwa
adhima ya kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati kutokana na viwanda
itatimia endapo wafanyabiashara wenye viwanda watakua wazalendo kama
Bakhresa.
Naye
Mwakilishi wa Kampuni ya Bakhresa Food Production Ltd Bw. Yusuph
Bakhresa ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara
wenye viwanda nchini, hali ambayo itasaidia kufikia lengo la Serikali ya
Awamu ya Tano ya kuitaka Tanzania kuwa nchi yenye viwanda ifikapo mwaka
2025.
Na Frank Shija, MAELEZO
|
October 7, 2016
JPM ATAKA TANESCO KUPELEKA UMEME KIWANDA CHA BAKHRESA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment