![]() |
Wizara
ya Mambo ya Katiba na Sheria imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa
kushirikiana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kujihusisha
kikamilifu na upelelezi wa kesi ya mauaji ya wataalamu wawili wa utafiti
wa udongo na dereva mmoja, yaliyotokea hivi karibuni katika kijiji cha
Iringa Mvumi wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma.
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema wizara
yake itahakikisha kuwa wote waliohusika kufanya tukio hilo la mauaji
wanafikishwa mahakamani.
Na
kwamba, Jamhuri itahakikisha inadai adhabu kali kwa kila mtuhumiwa ili
kutoa fundisho kwa wananchi wote kwamba tabia ya kujichukulia sheria
mkononi kwa kigezo cha hasira kali hakifai.
“Ili
kukomesha kabisa wimbi hili la wananchi kujichukulia sheria mkononi ,
wizara itachukua kila hatua inayowezekana kuhakikisa kuwa wote
waliohusika kushawishi, kuhamasisha, au kuchochea ,kupanga, kushambulia
kwa mapanga na kushiriki kuchoma moto katika tukio hilo wanafikishwa
mahakamani kuvuna walichopanda,” amesema.
Dk.
Mwakyembe amesema wizara inashtushwa na ongezeko la matukio ya wananchi
kujichukulia sheria mkononi kwa visingizio mbalimbali.
“Wengi
wanafanya matukio hayo kwa visingizio mbalimbali kama kukasirishwa na
baadhi ya matukio wanayoyaona mabaya, kuhisi kuonewa, kuchoshwa na
michakato halali ya kisheria ya upelelezi, uendeshaji kesi na utoaji
hukumu,” amesema.
Amevitaka vyombo vya habari kuisaidia serikali katika kampeni ya kutokomeza vitendo vya wanachi kujichukulia sheria mkononi.
“Wizara
inavitaka vyombo vya habari kubadilisha mfumo wa kuripoti matukio kama
hayo kwa kuachana na maneno kama wananchi wenye hasira kali ambayo ni
kisingizio kinachowafanya baadhi ya watu kufanys matukio hayo,” amesema.
|
October 7, 2016
DCI NA DPP KUCHUNGUZA MAUAJI YA WATAFITI DODOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment