
Taasisi
ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) inaendelea na
kongamano lake la kimataifa la Wanasayansi watafiti la 30 jijini Dar es
Salaam.
…………………………………………………….
Miongoni
mwa mambo mengi ambayo yajnajadiliwa ni pamoja na namna ya kuweza
kuhamasisha na kusaidia watoto wa kike nchini kuweza kusoma masomo ya
sayansi na kuwapa hamasa za kuweza kutimiza ndoto zao kufikia malengo
hayo.
Wanawake
wanasayansi watafiti walikutana na kujadili namna yakuweza kusaidia
kuleta hamasa kwa watafiti chipukizi na wale walioko shulebni kuweza
kuvutiwa na masomo ya sayansi na kusoma kwa bidii.
Pichani
juu ni Mwanasanasi Mtafiti Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Amani Tanga, Dk Theresia Nkya akielezea
chagangamoto mbalimbali alizokumbana nazo na namna
alivyoweza kuzikabili hadi kutimiza malengo yake.
alivyoweza kuzikabili hadi kutimiza malengo yake.
Mwisho
wa mdahao huo watafiti hao kila mmoja aliweka ahadi yake kimaandishi
jinsi ambavyo atasaidia kwa nafasi yake wale ambao wanachipukia na
kutaka kuchukua masomo ya sayansi waje kuwa watafiti.
Aidha
watafiti hao wanasayansi wanawake wametaka kuwepo na mikakati endelevu
ya kuweza kuwasaidia wanasayansi chipukizi ili uhamasishaji unaofanyika
mashu;leni kuwataka watoto wakike kusoma masomo ya sayansi uwe na
mafanikio na kuleta tija.
Mwanasayansi
Mtafiti kutoka NIMR Makao Makuu, Basiliana Emidi nae akitoa ushuhuda
wake kwa yale aliyopitia na anayopitia na ushauri wake kwa wanasayansi
wanawake chipukizi.
Mwanasayansi
Mtafiti Mstaafu, Dk Edith Lyimo nae alipata wasaa wa kuzungumza na
kuelezea yale aliyokumbana nayo wakati akifanya tafiti mbalimbali na
jisni alivyofanya kazi zake na wanaume miaka ya 1980.
Dk Nkya aliwataka wanasayansi watafiti chipukizi kuto kata tamaa na badala yake kuhakikisha wanafikia malengo yao kikamilifu.
Tunu
Mwinyimbegu (katikati) ni mmoja kati ya wasichana ambao wanandoto za
kuwa wanasayansi watafiti licha ya kuwa alikuwa na vitu vingine
alivyokuwa akifikiria kuvifanya katika maisha yake kama vile kuwa
msanifu kurasa akieleza ndoto zake na watu wanaompa hamasa. Kulia ni
Lucy Mrema na kustoto ni Mary-Angel Jimmy wote kutoka Taasisi ya Umoja
wa Mataifa ya Mahakama ya Makosa ya Jinai (MICT).
Mary-Angel
Jimmy wote kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mahakama ya Makosa ya
Jinai (MICT) akielezea ndoto zake za kuwa mwanasayansi na watu
wanaomsukuma kutimiza ndoto hizo.


No comments:
Post a Comment