Kikosi
cha kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) kupitia kwa Mwenyekiti wake wa
Kikosi hicho KMKM Sports Club, Kapteni Khatib Khamis Mwadini
amebainisha kuwa, mbio hio za Kilomita 10 zitakazofanyika tarehe 29
mwezi huu zinatarajia kuanzia Makao Makuu ya kikosi hicho Kibweni na
kumalizikia Uwanaja wa Maisara Mjini Zanzibar.
Na kuongeza kuwa, tayari maandalizi yanaendelea huku taratibu zote zikiwa zimesha fuatwa.
Mwenyekiti
wa Kikosi cha Kuzuia Magenzo Zanzibar (KMKM) Sports Club Kapteni Khatib
Khamis Mwadini akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mbio za
Kilomita 10 zitakazofanyika tarehe 29 mwezi huu kuanzia Makao Makuu ya
kikosi hicho Kibweni na kumalizikia Uwanaja wa Maisara Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Chama cha riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas akitoa maelekezo juu ya
mbio za Kilomita 10 zilizoandaliwa na Kikosi cha KMKM katika Mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni.
Mwenyekiti
wa Kamati ya ufundi wa mbio za Kilomita 10 za KMKM Luteni Mlingi Mganga
Bwire akijibu maswala yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika
mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Kikosi cha Kuzuia Magenzo Zanzibar (KMKM) Sports Club Kapteni Khatib
Khamis Mwadini akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani).
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar


No comments:
Post a Comment