![]() |
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo, amewasimamisha kazi watumishi
watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhirifu
wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015.
Watumishi
hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa msimamizi wa uchaguzi
wa mwaka 2015 na kumfuta cheo hicho, bwana Evansi Mwalukasa alikuwa
mwekahazina wa halmashauri na bwana Sembeli Sinayo yeye alikuwa
mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi
hayo yamefikia baada yakubainika kuna upotevu wa fedha za uchagu
takribani Milioni 188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa wazi na pia
Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata taratibu za
manunuzi ya serikali.
“Kuanzi
sasa nawasimamisha kazi hawa watumishi watatu kwasababu wameisababishia
serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha za
uchaguzi,” alisema Gambo.
Aidha
Muheshimiwa Gambo alisema maamuzi hayo yametokana na taarifa
aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda yakuchunguza mapato na matumizi ya
fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi ambazo
zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Ambapo
fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi ambayo hayakufuata taratibu
na sheria za manunuzi ya serikali, hivyo ni kinyume kabisa na taratibu
za serikali katika maswala ya manunuzi.
Akisisitiza
kwa watumishi wa serikali kufuata taratibu, sheria na kanuni mbalimbali
katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano na uvunjifu wa
sheria mahala pa kazi nakupelekea kupoteza kazi zao.
|
October 5, 2016
RC ARUSHA ASIMAMISHA WABADHIRIFU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment