Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Baada ya kufanyika kazi ya ziada ya kumshawishi Kocha Hans Van
Der Pluijm kurejea kuifundisha Yanga anatarajia kusimama kwenye benchi
la ufundi dhidi ya wabishi wa Mwanza Mbao FC kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam.
Pluijm
raia wa Uholanzi aliamua kuandika barua kuachia ngazi, lakini uongozi
wa Yanga ukamuangukia na kumfanya abadili uamuzi wake huo.
“Najua
itakuwa mechi ngumu, timu zote zinajiandaa na inakuwa faraja kwao
kushinda dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa kwani niliwaona kwenye mechi
yao na Simba waliwakomalia”alisema Pluijm.
Aidha
amesisitiza kuwa Wachezaji wangu wako tayari na wanajua sisi ni kina
nani na wanaocheza na sisi wanataka nini tutaingia kwa kauli moja tu ni
kupata alama tatu muhimu kwani hakuna kulala.
Yanga
imeonyesha kurejea katika kiwango chake kwa kushinda mabao kumi katika
kila mechi, ikianza na kuitandika Kagera Sugar mabao 6-2 na JKT Ruvu
mabao 4-0.
Na mpaka sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na
alama 24 kwa michezo 11 na ikizidiwa alama 8 na vinara Simba wenye alama
32 mechi 12.


No comments:
Post a Comment