
Na.Alex Mathias.
Uongozi wa timu ya soka ya Kagera Sugar umesema kwamba bado una
inami na kocha mkuu wa klabu hiyo Mecky Mexme licha ya baadhi ya
mashabiki kuonyesha mabango ya kutokuwa na imani nae ya kuendelea
kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Mwenyekiti wa Kagera Sugar
Salum Madaki, amesema kuwa kwanza anashangazwa na mashabiki wa timu hiyo
kudiriki kubeba mabango ambayo hayana msingi kwani kwa hali ilivyo
kocha wao anastahili kupewa sifa kwa jitihada kubwa alizozifanya za
kuhakikisha timu bado ipo katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi
tofauti na msimu uliopita.
Madaki amesema kuwa mashabiki
wa timu hiyo wasigetemee kuondoka kwa Mexme ndani ya kikosi hicho kwa
wakati huu kwani uongozi bado unaridhishwa na ufundishaji wake licha ya
kupoteza michezo miwili mfululizo ikiwemo dhidi ya Azam ambapo
walikubali kufungwa kwa jumla ya mabao 3-2 huku wakiwa wametoka kufungwa
na Yanga mabao 6-2.
Na Mpaka sasa Kagera Sugar ipo nafasi ya tano wakiwa na alama
18 na tofauti na Msimu uliopita kwani ilijinasuwa kushuka daraja hivyo
mashabiki watulie kwani Mexime ni kocha bora hapa nchini Tanzania.


No comments:
Post a Comment