KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 30, 2016

TIMU YA KRC GENK YA SAMATTA YAPATA USHINDI

samatta
Timu ya KRC Genk imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Westerlo mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji inayojulikana ‘Jupiler League mechi hii imechezwa kwenye uwanja wa Laminus Arena. Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafunga kutokana na uimara wa ulinzi pamoja na washambuliaji kutokuwa makini wanapopata nafasi ya kufunga.
Dakika ya 54 Genk walipata bao la kwanza kupitia kwa Alejandro Pozuelo akipokea pasi safi kupitia Leon Bailey na 66 mshambuliaji anayemuweka benchi Samatta Nikos Karelis alifunga la pili naye akipokea mpira toka kwa Mjamaica Leon Bailey aliye kwenye fomu ya hali ya juu.
Baada ya kufunga bao Karelis alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbwana Ally Samatta na katika dakika ya 82,Jamo Molenberghs aliifungia Westerlo bao la kufutia machozi hadi kipyenga kina pulizwa Genk wameibuka na ushindi wa mabao 2-1. Aidha huo unakuwa mchezo wa 31 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 12 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita. Katika mechi hizo, ni 16 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 14 alitokea benchi nane msimu uliopita na 11 msimu huu na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
Kwa matokeo hayo KRC Genk wamepanda hadi nafasi ya 6 katika msimamo wa Jupiler League wakiwa na alama 20 huku wakiwa wameruhusu kufungwa mabao 18 na wao wakiwa wamefunga mabao 17 na wakiwa wamecheza jumla ya mechi 13,sare miwili,kufungwa michezo mitano na kushinda sita

No comments:

Post a Comment