Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Bunge Bw.Uledi Mussa amesema kuwa wabunge
wana uhuru mkubwa sana wa kuzungumza ndani ya Bunge.
Katibu Mkuu uyo ameyasema hayo
katika kipindi cha TUNATEKELEZA leo jioni kinachoandaliwa na Idara ya
Habari MAELEZO na kurushwa na TBC1.
“Bunge letu liko huru sana,liko
huru kwa maana wabunge wana uhuru wa kuzungumza na kikatiba yale
wanayozungumza ndani ya bunge hawawezi kushitakiwa nje,kwa maana hiyo
kuna uhuru mkubwa sana,lakini sasa bunge lenyewe lina Kanuni zake ambapo
wewe uliye ndani ya Bunge usimseme mtu ambaye hana fursa ya kuzungumza
ndani ya Bunge hivyo bungeni msingi wake mkubwa ni kuzungumza hoja
pamoja na kuikosoa,kuishauri serikali na tunafatilia ushauri huu kisekta
ili ufanyiwe kazi”Alisema Bw.Uledi
Akizungumzia suala la utoro
Bungeni amesema kuwa kwa sasa mahudhurio yanaratibiwa kielektronikali na
wabunge watapaswa kuweka dole gumba kwenye mshine ili ajulikane
kaingia na kutoka na baadae mahudhurio hayo uchambuliwa na kutumwa
katika vyama vyao na hivyo ili litaongeza uwajibikaji binafsi kwa
wabunge.
Akizungumzia upande wa hali ya
vyama vya siasa nchini katibu mkuu uyo amesema kuwa vyama vingi vya
siasa bado ni vichanga na msingi wa vyama vingi hauna muda mrefu hivyo
bado vina kazi kubwa ya kujijenga vyenyewe kama taasisi kwenye kuchagua
viongozi na Katiba zao.
Aidha katibu Mkuu uyo amevitaka
vyama vya siasa kujenga misingi ya kukubali matokeo ya chaguzi
zinapofanyika na pia vijenge umoja unaozingatia katiba za vyama vyao.
Bw,Uledi pia amesisitiza kuwa
matatizo yanayotokea ndani ya vyama vya siasa yanapaswa kutatuliwa na
vyama na wanachama wao wenyewe na kuongeza kuwa migogoro mingi ndani ya
vyama ni ya kikatiba na hivyo wasitegemee mtu kutoka nje aje
kuwatatulia matatizo yao ingawa ofisi ya waziri mkuu itaendelea
kushirikiana na msajili wa vyama vya siasa katika kuwa mlezi wa vyama
hivi.



No comments:
Post a Comment