Na.Alex Mathias,Dar es salaam.Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaomba wanachama wa timu hiyo kuwa watulivu mara baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, kuzuia mkutano wa dharura uliopangwa kufanyika kesho kwenye makao makuu ya klabu hiyo.
Akizungumza
na waandishi Leo amesema kuwa ni kweli jana jioni walipata barua kutoka
mahakama hiyo ya kuzuia mkutano ambao ulikuwa halali kikatba ya Yanga.
“
Tuwaombe radhi kwa wanachama wote kutoka sehemu mbalimbali kwa gharama
zenu hata kama waliozuia mkutano wetu si wanachama na tunaamini itafikia
siku, tutakutana kwa kuwa mkutano ni haki yetu ya msingi”alisema Manji.
Aidha
amesema kuwa utulivu ni jambo jema, lazima tuonyeshe ukweli kuwa sisi
ni watulivu, waelewa lakini tutekeleze uamuzi huo wa mahakama huku
tukisubiri siku yetu itafikia na kila kitu kitafanyika kwa utaratibu.
Hata
hivyo, Manji alisema waliopeleka zuio hilo la mkutano si wanachama kwa
kuwa Frank Chacha hajalipia ada yake kwa zaidi ya miezi sita na mwingine
Juma Magoma pia si mwanachama wa Yanga kwa kitambo sasa.
Aidha,
alisisitiza hata hao waliokwenda mahakamani kama wangekuwa wanachama
hai, basi wangekuwa wameishajifuta rasmi baada ya kwenda mahakamani kwa
kuwa katiba ya Yanga inakataza kwenda mahakamani kama ilivyo kwa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Klabu
ya Yanga ilitarajia kufanya Mkutano Mkuu wa dharura wa kujadili
mabadiliko yanayotaka kufanyika kwenye mwenyekiti huyu kukodishiwa nembo
ya klabu hiyo kwa miaka 10 jambo ambalo limeanza kugawa wanachama ambao
wengine wanataka akodishiwe na wanaopiga.


No comments:
Post a Comment