![]() |
| Mateka hao waliachiliwa huru wikendi na wakafika Kenya Jumapili.
Kundi la mabaharia ambao
waliachiliwa huru Jumamosi baada ya kuzuiliwa na maharamia kwa miaka
mitano nchini Somalia walikula hata panya ili waishi, mmoja wao ameambia
BBC.
Arnel Balbero, kutoka Ufilipino amesema walikuwa wanapewa
maji kidogo sana na walijihisi kama "wafu waliokuwa wakitembea" kufikia
wakati wa kuachiliwa huru kwao.Mabaharia hao walitekwa wakiwa kwenye meli mwaka 2012 kwenye pwani ya Ushelisheli na wakapelekwa Somalia bara na kuzuiliwa mateka. Waliachiliwa huru Jumamosi. Taarifa zinasema waliokuwa wanawazuilia mateka walilipwa kikombozi.BBC |
October 24, 2016
MATEKA WASEMA WALIKULA PANYA SOMALIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment