![]() |
Maafisa wa kampeni wa mgombea urais
wa chama cha Republican nchini Donald Trump wamekiri kwamba mgombea huyo
yupo nyuma ya mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democratic
zikiwa zimesalia chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika.
"Tuko nyuma. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanamfaa yeye (Bi Clinton)," meneja wa kampeni wa Bw Trump, Kellyanne Conway amesema.Hata hivyo, ameongeza: "Hatukati tamaa. Tunajua kwamba tunaweza kushinda." Mnamo Ijumaa, Bw Trump alionekana kukiri uwezekano kwamba anaweza kushindwa. Alisema iwapo atashinda, ashindwe au atoshane nguvu na mpinzani wake, ataridhishwa na juhudi zake. Siku moja baadaye, alitangaza hatua ambazo atazichukua siku 100 akiwa uongozini iwapo atashinda. Miongoni mwa hizo ni kuweka masharti mapya kwenye mchakato wa kisiasa wa kutafuta uungwaji mkono kisiasa, mikataba ya kibiashara na mabadiliko ya tabia nchi. Kura mpya za maoni zinaonesha Bi Clinton yupo mbele sana kitaifa na katika majimbo mengi yanayoshindaniwa. Maafisa wake kampeni wa Clinton wamebashiri kwamba huu utakuwa "uchaguzi mkubwa zaidi katika historia ya Marekani".BBC |
October 24, 2016
TRUMP-TUKO NYUMA LAKINI HATUKATI TAMAA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment