Mwaka 2014 ZESCO
ilimsaini Lwandamina kuwa kocha mkuu, katika msimu wake wa kwanza
aliisaidia ZESCO kutwaa taji la ligi kuu ya Zambia kisha kulitetea msimu
uliofuta. (Picha na Mwananchi Communications Ltd)
Taarifa inayosambaa kwa
kasi kwenye mitandao ya kijamii ni ujio wa kocha mpya George Lwandamina
anayetajwa kuchukua nafasi ya Babu Hans van der Pluijm kwenye kikosi cha
Yanga SC.
Jana iliripotiwa kocha
huyo ameshatua jijini Dar kwa ajili ya kumaliza taratibu za kukabidhiwa
mikoba kutoka kwa Mholanzi Van Pluijm, lakini taarifa iliyopo sasa ni
kwamba, Lwandamina tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha
klabu ya Yanga.
Awali ilielezwa kuwa,
baada ya kocha huyo mzambia kupewa majukumu ya kukinoa kikosi cha Yanga,
Pluijm atakuwa Mkurugenzi wa ufundi wa mabingwa hao watetezi wa taji la
VPL. Taarifa zilizopo ni kwamba klabu ya Yanga itamleta Mkurugenzi wa
ufundi kutoka nchini Ureno.CHANZO BLOG YA WANANCHI



No comments:
Post a Comment