
Wataalamu wa Masuala ya Uchumi
na Fedha kutoka Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia
na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakifuatilia mazungumzo ya mkutano
kati ya Shirika la Fedha Duniani-IMF na Wizara ya Fedha na Mipango,
mkutano uliofanyika katika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini
Washington DC, Marekani.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakiwa katika
kikao cha kazi na uongozi wa juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, ambapo
masuala kadhaa yanayohusu hali ya uchumi na maendeleo ya miradi
inayofadhiliwa na shirika hilo ilijadiliwa, Mkutano huo umefanyika
katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa tatu kutoka kushoto)
akiwa kwenye mkutano na Magavana kutoka nchi mbalimbali za kiafrika
wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha
Duniani-IMF, Jijini Washington DC nchini Marekani, akielezea juu ya
ukuaji wa uchumi katika shughuli za mawasiliano, madini, huduma ya
fedha, bima na huduma za uzalishaji wa viwandani pamoja na changamoto
zilizopo..

Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt.
Natu A. Mwamba akifafanua juu ya changamoto zinazoikumba Tanzania katika
kukuza uchumi hasa katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu, akiwa
mmoja wa wachokoza mada wengine kutoka nchi kadhaa za Kiafrika kwenye
mkutano uliojadili kuhusu hali ya Afrika, Jijini Washington DC
–Marekani.


No comments:
Post a Comment