KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 25, 2016

MOROCCO KUJENGA UWANJA WA MPIRA DODOMA

16
Rais Dk. John Pombwe Magufuli akizungumza Ikulu jana kuhusu mgeni wake Mfalme Mohammed VI anayemsikiliza kukubali kujenga uwanja mkubwa wa michezo mkoani Dodoma pamoja na msikiti mkubwa jijini Dar es salaam a ukiacha mikataba zaidi ya 20 ya kibiashara iliyosainiwa jana kati ya makampuni ya Tanzania na Morocco Ikulu jijini Dar es salaam.
(PICHA NA HASSAN SILAYO -MAELEZO)
……………………………………………………………….
Na Daudi Manongi; MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na Mfalme Mohamed  wa Sita  wa Morocco kujenga Uwanja wa Mpira wa miguu wa  kisasa mkoani Dodoma utakaogharimu dola milioni 100.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kutiliana saini kwa mikataba 21 ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Morocco.
“Mbali na mikataba baina ya Tanzania na Morocco nimezungumza mambo mbalimbali na Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco na nimemuomba atujengee Uwanja mkubwa wa mpira pale Makao Makuu yetu Dodoma utakaokuwa na thamani kati ya dola milioni 80 hadi  100 na amesema ataujenga, kwa hiyo utakuwa Uwanja mkubwa kuliko wa Dar es Salaam”. Alisema Rais Magufuli.
Mbali na hayo Rais Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara wa Morocco kuwa Tanzania ni salama na inapenda kushirikiana nao, na kuwa nchi yetu iko katika mwelekeo mzuri wa uwekezaji ambapo uchumi wa nchi yetu unategemea kukua kwa asilimia 7.2 mwishoni mwa mwaka.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw.Salahddine Mezour ameishukuru nchi ya Tanzania kwa ushirikiano iliounyesha na kusema kuwa Morocco itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali kwa kuwa ina utulivu wa kisiasa na icho ndo kimekuwa kivutio kikubwa katika kuwekeza kwao nchini hapa.
Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais, Dk John Pombe Magufuli ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili na kutiliana saini mikataba 21 ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment