
Wanamuziki wa bendi ya Msondo
Ngoma Shaban Dede kulia na Hassan Moshi wakiimba jukwaani katika moja ya
maonesho ya bendi hiyo jijini Dar es salaam.

Katibu wa kamati ya maandalizi ya Maonyesho hayo ya kila mwezi Bw.Abdulfareed Hussein
…………………………………………………………………………..
Bendi kongwe ya muziki wa dansi
nchini,MSONDO NGOMA MUSIC BAND(BABA YA MUZIKI),inakuletea onyesho lao
kubwa la kila mwezi maalum kwa wanafamilia wa Msondo Ngoma na wadau wa
muziki wa dansi maarufu kwa jina la MSONDO NGOMA FAMILY DAY,ambalo kwa
mwezi huu litafanyika wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Lekham
Hotel,Buguruni.
Akiongea na fullshangwe
blog,Seneta wa Bendi hiyo ambaye pia ni katibu wa kamati ya maandalizi
ya Maonyesho hayo ya kila mwezi Bw.Abdulfareed Hussein,ameeleza kwamba
baada ya mafanikio makubwa katika maonyesho yalopita,sasa burudani
itaangushwa Lekham Hotel,ikiwa na kauli mbiu ya CHANGIA BENDI
YAKO,CHANGIA BIMA YA AFYA KWA WANAMUZIKI WETU.
Katibu huyo pia amefafanua kwamba
onyesho la mwezi huu litakuwa maalum la kuchangia upatikanaji wa bima
ya afya kwa wanamuziki wa Msondo ngoma.
Bendi hiyo imedhamiria kuja na
mipango mbalimbali katika kuendeleza muziki wa dansi na kadri siku
zinavyokwenda ndivyo mikakati mbalimbali itakavyotekelezwa.
Katika onesho hilo pia kutakuwa
na zawadi kwa mtu atakayecheza vizuri mtindo wa msondo ngoma ,
atakayeimba vizuri nyimbo ya mashindano ya Msondo Ngoma na
atakayependeza zadi katika siku hiyo.
Kiingilio katika onyesho hilo
kitakuwa ni 10,000,japo wadau wanaruhusiwa kuchangia zaidi ya bei hiyo
na kwa mawasiliano ya uchangiaji wa awali unaweza kumpata na kukupa
maekekezo kupitia namba ya simu 0653909050.
CHANGIA MSONDO NGOMA,CHANGIA BIMA YA AFYA KWA WANAMUZIKI WETU.


No comments:
Post a Comment