Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo leo ametekeleza agizo la Rais
Magufuli la kusitisha safari ya kwenda Mkoani Simiyu kwenye sherehe za
kuhitimisha kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru kwa kurejesha kiasi cha
Jumla ya Shilingi 1,389,300.
Fedha hizo yalikuwa ni malipo kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa, Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa , Dereva wa Mkuu wa Mkoa na gharama za mafuta.
Akiongea
na mwandishi huyu ofisini kwake leo, mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha
amesema wakati agizo hilo linatolewa yeye alikuwa bado hajaanza safari
ya kuelekea mkoani Simiyu, na kwamba amelipokea bila kinyongo na mara
moja akaamua kurejesha posho hiyo, akionesha stakabadhi ya kuthibitisha
hilo.
Kwa
mujibu wa mchakato wa malipo ya posho kwa safari hiyo ya kwenda mkoani
Simiyu kwa siku tatu, posho ya RC ilikuwa ni Sh 360,000, Msaidizi wa RC
Sh 240,000, posho ya dereva 24,000 na Sh 549,300 kwa ajili ya Mafuta ya
gari.


No comments:
Post a Comment