Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeagiza taasisi na mashirika yote yasiyo ya kiserikali (NGO’s)
yanayohusika na utoaji wa elimu ya Ukimwi kusitisha huduma hizo hadi
itakapo toa muongozo mpya wa utoaji huduma katika ngazi ya jamii.
Waziri
wa Wizara ya Afya, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, alisema kumekuwepo na ongezeko kubwa la
NGO’s ambazo zinasababisha muingiliano katika utoaji huduma za kijamii
pamoja na kufanya kazi katika mikoa michache, ambapo amemuagiza Mganga
Mkuu wa Serikali kuzipangia mikoa taasisi zinazotaka kufanya kazi.
“Serikali
inaendelea kuzuia utolewaji wa huduma hizo kwa ngazi ya jamii hadi pale
ambapo wizara itapitia mwongozo mpya wa utoaji huduma ngazi za kijamii
kwa makundi maalumu. Shughuli za NGO’s kwenda kwa jamii kugawa
vilainishi au kutoa elimu zitasimama hadi itakapotolewa mwongozo mpya wa
utoaji huduma kwa jamii,” alisema.
Amesema
wizara imeweka utaratibu mpya wa kusajili taasisi hizo na kwamba kabla
ya kuanza kufanya kazi zinatakiwa kutoa taarifa kwa mkurugenzi wa
halmashauri anayotaka kufanyia kazi.
“Kumekuwepo
na ongezeko kubwa la idadi ya wadau wanaohitaji kusaidia serikali, ili
kuleta huduma hizo kwa ngazi ya jamii, na kwamba ili kuleta tija,
uwajibikaji na uwazi katika utolewaji wa huduma hizo, mganga mkuu wa
serikali atawapanga wadau katika mikoa kulingana na idadi yao,” alisema.
Amesema NGO’s hizo zinatakiwa kutambuliwa na halmashauri husika kabla ya kuanza kazi.
“Mkurugenzi
wa halmashauri atatambulisha wadau au NGOs na kutia kibali, tunazuia
asasi hizi kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kufanya kazi pasipo
kuthibitishwa na wamurugenzi wa halmashauri,” alisema.
Kutasainiwa
makubaliano ya kufanya kazi kusudi muweke makubaliano ya namna ya
ufanyaji kazi. Lengo letu kumsaidia waziri wa katiba na sheria, hatutaki
watu kuitumia wizara ya afya kukiuka sheria kwa kigezo cha kusaidia
jamii.
No comments:
Post a Comment