KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 26, 2016

TBL KUZALISHA KWA UMEME WA JUA

 Katika mkakati wake wa kufanya uwekezaji wa mitambo inayotumia teknolojia ya kisasa na kufanya uzalishaji usiochafua mazingira,kampuni ya TBL Group imeanza kufanya uzalishaji wa bia kwa kutumia umeme unaotokana na nishati ya jua.
Uzalishaji wa kutumia umeme wa jua umeanza mapema wiki hii katika kiwanda cha bia cha Mbeya baada ya kukamilika kwa zoezi la kufunga vifaa vya kuvuna umeme wa jua kwenye kiwanda hicho vyenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kilowati 138.
Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni hiyo,Gavin Van Wijk, amesema kuwa teknolojia ya matumizi ya umeme unaotokana na nishati ya jua kuendesha kiwanda kikubwa kama hicho ni mpya hapa nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema mitambo hiyo ya umeme wa jua imetengenezwa nchini Ujerumani na ina uwezo wa kuzalisha Kilowatt 138 na inao uwezo wa kukidhi mahitaji ya matumizi ya umeme wa kiwanda kwa asilimia zaidi ya 30%.solar-panel-3

No comments:

Post a Comment