Wizara
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imezifuta shule
nyingine za awali na msingi nchini ambazo hazijasajiliwa zaidi ya 10
kuanzia Desemba mwaka jana. Aidha, shule tano kati ya 40 zilizokuwa
zimefutiwa usajili zimekamilisha taratibu na kurejeshewa usajili wake.
Kaimu
Mkurugenzi wa Usajili wa Shule katika wizara hiyo, Khadija Mcheka
amesema mpaka sasa bado wanaendelea na ukaguzi kubaini shule ambazo
hazijasajiliwa.
Alizitaja
shule ambazo zimefutwa kwa kutosajiliwa kuwa ni Mwandai Junior Academy,
shule ya msingi DACETE, shule za msingi Malaika na Fares Kisingo (FK)
za wilaya ya Kinondoni. Nyingine ni shule ya msingi The Unity, shule ya
sekondari Jotac iliyopo eneo la Kipunguni, Verena iliyopo eneo la Pugu
zote wilaya ya Ilala, Exodus iliyopo Kigamboni na Havard Junior ya
wilaya ya Temeke.
Alisema
shule nyingine zilizofutwa kabisa ni shule ya sekondari ya Kahe ambayo
imefutwa kutokana na wamiliki kushindwa kuiendesha na pia majengo yake
yamebadilishiwa matumizi.
Alisema
shule nyingine za Deogrolius International School iliyopo Kitunda,
Desinity na Almustakim zote za jijini Dar es Salaam nazo zimefutiwa
usajili. Alisema awali yalitolewa majina ya wamiliki.
Mcheka alisema pia shule mbili hazitakiwi kuwa za bweni ambazo ni Heritage iliyopo Banana Ukonga na Hellens iliyopo Kinondoni.
Akizungumzia
shule zilizorejeshewa usajili, alisema ni Gisera, Rose Land, Conerstone
na Grace za jijini Dar es Salaam na Must Lead na Qunu zilizopo mkoani
Pwani huku shule ya Fountain Gate ikifutiwa usajili wa kuendesha
shughuli za bweni.
Akifafanua
kuhusu shule ya Coner Stone alisema baada ya ukaguzi na kufutiwa
usajili kuanzia mwezi Julai zipo shule ambazo zilikamilisha utaratibu na
kurejeshewa usajili, na kwamba hakuna shule iliyoelezwa kufutiwa
usajili kwa uongo.
“Kuhusu
shule zinazolalamika kutangazwa kimakosa si kweli isipokuwa jambo
lililofanyika baada ya kuwapelekea barua kuwataka kutawanya wanafunzi
baada ya kufutiwa usajili walikamilisha utaratibu ndipo wakasajiliwa,“ alisisitiza.
Alisema
ukaguzi huo wa shule unaendelea katika mikoa yote nchini kwa kuwatumia
wakaguzi wa Kanda na watakaobainika watafutwa mpaka watakapokidhi vigezo
vinavyotakiwa.
Hivi
karibuni Mcheka alisema kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana,
waligundua kuwepo kwa shule 35 zisizosajiliwa na kuzifuta na baadaye
walizifungia shule nyingine 12.



No comments:
Post a Comment