
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati)
alipofanya ziara ya kukagua mazingira katika kiwanda cha kutengeneza
viroba vya mifuko Unberg International kilichopo jijini Dar es
salaam.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (kushoto) mara
baada ya kuwasili na kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga
cha Murzer kilichopo jijini Dar e s salaam.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akikagua sehemu ya
kuyeyushia viroba ya mifuko katika kiwanda cha Unberg International
kilichopo jijini Dar es salaam mapema hii leo.
………………………………………………………………………
EVELYN MKOKOI-DAR ES SALAAM
Shule ya sekondari ya Almuntazir
iliyopo upanga jijini Dae es salaam imetozwa faini ya shilingi milioni
ishirini na tano kwa kosa la uchafuzi wa mazingira kwa kutirirsha maji
taka ya chooni katika mto msimbazi ndani eneo la mikoko katika eneo la
daraja la salenda na kujenga uzio wa ukuta bila kuzingatia mita sitini
zinazotakiwa kisheria.
Faini hiyo inatakiwa kulipwa
ndani ya wiki moja imetokana na ziara ya Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina iliyofuatia malalamiko ya
wakazi wa Upanga iliyompelekea Naibu Waziri kufanya ziara yakwenda
kujionea uchafuzi huo.
Akiongea kwa Niaba ya shule
meneja wa shule hiyo Bw. Serialis Rwechungura amesema kuwa, watalipa
faini hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali na hakuwa tayari kuongelea
swala la ukuta wa shule hiyo.
Naibu Waziri Mpina amesisitiza
kuwa serikali haitakuwa tayari kuwavumila wawekeajia wakiukaji wa sheria
hasa ya mazingira, na kuweka rehani maisha ya watanzania.
Aidha Naibu Waziri alitembelea
maeneo ya mwenge kijijini na kuonea uchafu wa mazingira uliotokana na
kuvuja kwa maji taka ya choo kutoka kwenye miundombinu ya majitaka ya
DAWASCO hali inayosababibsha wakazi na wafanyabiashara wa maeneo ya
mwenge kushindwa kustahimili hali hiyo na kuwa hatarini kupata magonjwa
ya maambukizi kama kipindupindu na homa ya matumbo.
Akiikemea DAWASCO kwa mara
nyingine kwa kutokuonyesha uwajibikaji na utii kwa mamlaka za juu, Naibu
Waziri Mpina ameita NEMC kuiandikia DAWASCO faini ya shilingi milioni
ishirini na tano kwa kutelekeza miundombinu yao na kutakiwa kulipa
adhabu hiyo kwa muda wa wiki mbili.


No comments:
Post a Comment