
Mkurugenzi
wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, John
Mnali (Katikati), akibadilishana mawasiliano na mmoja wa
wafanyabiashara walioonesha nia ya kuweka nchini Tanzania baada ya
Mkurugenzi huyo kuwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji
zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa
kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini
Seoul, Korea Kusini.

Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akibadilishana
mawasiliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MarineBio, Heo
Yun-Young, ambaye kampuni yake inataka kuwekeza kiwanda cha kusindika
zao la mwani linalopatikana katika Bahari Kuu ya Hindi nchini Tanzania

Msaidizi
wa Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Makamba, akiwa katika picha ya
pamoja na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea
Kusini, Lee Duk-Hoon baada ya hafla ya usiku ya kuagana kwa washiriki wa
mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za
Kiafrika, Jijini Seoul, nchini Korea kusini.

Mkurugenzi
wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, John
Mnali, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana
Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya
Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini

Maofisa
kutoka wizara ya Fedha na Mipango, Edwin Makamba ambaye ni msaidizi wa
Waziri wa Fedha na MIpango, kushoto, na Mkuu wa idara ya Sera, Shogolo
Msangi, wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kuhusu fursa za uwekezaji
zilizopo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wakati wakati wa mkutano wa
5 wa ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika,
uliomalizika leo Jijini Seoul, Korea Kusini

Mkuu
wa kitengo cha utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,
Zanzibar, Sabra Issa Machano, akiwasilisha mada kuhusu fursa za
uwekezaji zinazopatikana Tanzania Zanzibar, wakati wa mkutano wa 5 wa
ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika
(KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.

Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Mkuu wa
kitengo cha utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,
Zanzibar, Sabra Issa Machano, baada ya akiwasilisha mada kuhusu fursa za
uwekezaji zinazopatikana Tanzania Zanzibar, wakati wa mkutano wa 5 wa
ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika
(KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.


No comments:
Post a Comment