
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus
Kinawiro akiwashukuru Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini
Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu na
kusema kuwa mahitaji kwa waathirika wa tetemeko la ardhi bado ni makubwa
na misaada inahitajika ili kuwasaida waathirika hao.

Mratibu
Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Burhan
Mohammed akitoa neno mwishoni mwa wiki mara baada ya ya kukabidhi msaada
wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na
tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Mkuu
wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro (katikati aliyevaa suti) akiwa
katika picha ya pamoja na wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions
Club ya jijini Mwanza mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula
kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la
ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)
………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba
Kamati
ya maafa mkoani Kagera imeendelea kupokea misaada kutoka kwa wadau
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kutoa michango yao kwa lengo la
kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililoathiri mkoa wa Kagera.
Akikabidhi
msaada uliotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini
Mwanza Mratibu Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Burhan Mohammed amesema kuwa wao
kama taasisi wamevutwa na kushikwa kwa moyo wa huruma na kuamua
kuchukua hatua ya kuwasidia majirani zao wa mkoa wa Kagera.
Sisi
sote ni Watanzania, tuliposikia wenzetu wamepatwa na matatizo, tumeamua
kutoa mchango wetu kwa kushirikiana na wanachama wenzetu ili kutoa
huduma za kuwapa chakula wenzetu wakati wa matatizo” alisema.
Taasisi
hiyo imetoa Mchele, chumvi, mafuta ya kula, Sabuni pamoja na katoni za
maji ya kunywa ambapo vyote kwa jumla vinathamani ya sh. milioni 22.
Aidha,
Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Lwelu ya mkoani Kagera wametoa
vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni 2.1 ikiwa ni pamoja na
sukari, unga na mchele.
Wadau
wengine waliotoa misaada ni kampuni ya Time to Help yenye makao makuu
ya jijini Dar es salama ambayo inayomilikiwa Waturuki wametoa mablanket
500.
Akipokea
misaada hiyo kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya Bukoba
Deodatus Kinawiro amewaeleza wadau hao taswira mzima ya hali ya maafa
katika mkoa Kagera ambapo amesema kuwa mahitaji kwa waathirika bado ni
makubwa.
Kwa
niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya Bw. Kinawiro amewashukuru wadau wote
wanaendelea kutoa misaada kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Kagera
ambao wameathirika wa tetemeko hilo na kuwataka wadau wengine kuendelea
michango ya hali na mali katika kukabiliana na hali ya maisha baada ya
tetemeko kutokea.


No comments:
Post a Comment