
Hussein Makame, NEC
Watanzania wengi hawaijui Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), majukumu yake na miongozo inayoongoza
uchaguzi, hali inayosababisha manung’uniko mengi na upotoshaji kwa umma
juu ya tume hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani wakati
akitoa tathmini ya elimu ya mpiga iliyotolewa hivi karibuni kwenye
Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)
uliofanyika wiki mbili zilizopita mjini Musoma.
Bw. Kailima alisema kutokana na
hali hiyo, NEC imeanza kutekeleza mkakati kabambe wa kutoa elimu ya
mpiga kura kupitia njia mbalimbali ikiwemo kushiriki kwenye maonesho na
mikutano inayojumuisha wadau muhimu wa uchaguzi.
Alisema kutokana na utekelezaji
huo wa mkakati wa elimu ya mpiga kura anaamini baada ya miaka mitano au
kumi ijayo Watanzania wataifahamu tume hiyo na kufanikisha chaguzi
zijazo bila ya manung’uniko na kwa mafanikio makubwa zaidi.
“Baada ya miaka 5 au 10 ijayo,
tunategemea kwanza watu wataijua Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa sababu
bila kumung’unya maneno watu hawaijui Tume ndio maana wanauliza “hivi
baada ya uchaguzi nyinyi tume mnafanya nini” alisema Bw. Kailima na
kuongeza kuwa:
“Sasa wakiijuia Tume na ule
uhalali wake, uiaminifu wa wananchi kwa NEC utaongezeka kwa kiwango
kikubwa sana, manung’uniko kwamba tume haitimizi wajibu wake yatapungua
kwa kiwango kikubwa ”
“Pili ule upotoshaji itapungua
kwa sababu wananchi watakuwa wameelewa kwa kiwango fulani kuhusu Tume,
taratibu za uchaguzi na wakishaelewa wewe ukienda na jambo lako
watakushangaa.”


No comments:
Post a Comment