Kampuni
ya TBL Group mwishoni mwa wiki imemkabidhi Waziri Mkuu,Mh.Kassim
Majaliwa shilingi milioni 100/- kwa ajili ya kusaidia waathirika wa
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,amesema kampuni yake imeguswa na janga
hili kubwa hapa nchini ambalo limesababisha vifo vya watu na kubomoa
makazi na miundo mbinu na inaungana na wadau wengine kusaidia waathirika
ili waweze kurejea katika hali zao za awali na kuendelea na maisha
yao ya kawaida.
“Tunaunga
mkono jitihada za serikali za kusaidia wahanga wa tukio la tetemeko la
ardhi mkoani Kagera.Tupo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu
walichonacho wakati serikali inafanya jitihada za kuhakikisha
wanaendelea kupata huduma za kijamii ambazo zimevurugwa na janga
hili”.Alisema Jarrin.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (kulia) akimkabidhi Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa (wa tatu kutoka kulia) hundi ya shilingi milioni 100/-kusaidia
waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.(Kushoto) ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani na Nje wa
kampuni hiyo,Georgia Mutagahywa na (wa pili kutoka kulia) ni Fabian
Mwakatuma –Mkuu wa kitengo cha Ugavi wa TBL Group.
Roberto
aliongeza kuwa moja ya sera ya TBL Group ni kusaidia jamii
inakofanyia biashara zake wakati wote na ndio maana mbali na kutoa
msaada huu wa majanga imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya kuleta
mabadiliko kwenye jamii hususani katika sekta ya afya,Mazingira na
maji,elimu na kilimo.
“Siku
zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za
kuboresha maisha ya wananchi kwa kufadhili miradi mbalimbali ya kijamii
ikiwemo kutoa misaada wakati anapojitokeza majanga kwenye jamii.
Kwa
upande wake,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alishukuru TBL Group,
makampuni yote na wadau wengine ambao wameonyesha moyo wa kusaidia
wahanga wa tetemeko la ardhi ambao wanahitaji msaada wa kukarabati na
kujenga makazi na miundombinu mingine.


No comments:
Post a Comment