Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu
kama (Simba Asiyefugika),amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha usiku
wa kuamkia leo huko maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam kutokana na
sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization
ya ngumi za kulipwa nchini PST Antony Lutta,ameiambia
‘Fullshangweblog’ kuwa taarifa walizozipata ingawa bado
hazijathibitishwa inaonyesha Thomas Mashali ameuwawa.
Lutta ameongeza kwamba marehemu enzi za
uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa sasa hatujui
nini kimempata ambapo mwili wake umekutwa maeneo ya Kimara jijini Dare s
salaam ukiwa na majeraha baada ya hapo ulichukuliwa na kupelekwa
kuhifadhiwa katika hospitali ya taifa muhimbili.
Marehemu Mashali kabla ya kifo chake
alikuwa acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi ,pigano ambalo
lilipangwa kufanyika mkoani morogoro siku ambayo bondia mwenzake Dullah
Mbabe alipangwa kucheza pigano la utangulizi.
Mashali ambaye jina lake la kuzaliwa
ni Christopher Fabian Mashali,aliyezaliwa Septemba 09 mwaka 1989,ameacha
rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa
KO,amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku
akitoka sare pigano moja tu.
No comments:
Post a Comment