
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar
kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza timu ya Toto African ‘Wana-kisha
mapanda’ wametuma salama kwa wana rambaramba Azam Fc mchezo wao
utakaopigwa Jumatano hiii.
Akizungumza Ramadhani Aiko,ametamba kuwa wana imani kuwa
watashinda mechi hiyo kutokana ushindi wa Mtibwa kuwapa morali wachezaji
pamoja na benchi nzima la ufundi huku wakichangizwa na uwepo wa
mashabiki.
“Tunajipanga kuchukua alama tatu muhimu katika mchezo wetu na
Azam hivyo tuna tuma salama mapema kuwa wajiandaa kula kichapo kwani
tulianza kufunga na Mtibwa goli mbili hata hivyo vijana walijipanga na
kupigana na kurudisha na kupata ushindi wa 3-2″alisema Aiko
Toto walitoka nyuma ya kufungwa magoli mawili na wakata miwa
na waliporudi walikuja kupigana na hatimaye kushinda hivyo mchezo
utakuwa mkali na wa upinzani kwa timu zote mbili ukiangalia hata Azam
nao wametoka kushinda magoli 3-2 dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa
Kaitaba.
Kwa upande wa Msemaji wa Azam Jafar Maganga,ametamba kuwa nia
yao ni kupata alama tatu na malengo yao ni kuchukua pointi zote tisa
wakiwa kanda ya ziwa na mchezo na Toto watashinda japokuwa sio rahisi.
“Tumejipa kuwafunga Toto wakiwa hapo kwao kama tuliweza
kupata ushindi dhidi ya Kagera hivyo tunajua wapinzani wetu wanacheza
vipi na wakiwa nyumbani wanaonekana wangumu mpira ni dakika 90 sisi
tumejiandaa kushinda tunasubiri siku ifike tu”alisema Maganga
Azam Fc wanakutana na Toto wakiwa nafasi ya nne wakiwa na alama 19 wakati Toto wao wapo nafasi ya 15 na alama zao 11.
No comments:
Post a Comment