Na Lulu Mussa, Tabora
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na
Mazingira Mhe. Jauary Makamba amempongeza Bw. Leordard Kushoka kwa
kubuni kiwanda kinachotengeza nishati mbadala rafiki kwa mazingira.
Akiwa
Mkoani Tabora, Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea kiwanda hicho
na kusema kuwa Serikali inathamini sana ubunifu na uvumbuzi hasa unao
okoa mazingira. “Bwana Kushoka mimi nakupongeza sana, niliona jitihada
zako kupitia kipindi cha televisheni na kuamua kukuita na kukusaidia”
alisisitiza Waziri Makamba.
Katika
kuthamini mchango wa Kiwanda hicho cha “Kuja na Kushoka” Ofisi ya
Makamu wa Rais imemsaidia Bw. Kushoka kupata haki miliki ya Kiwanda
hicho.
Awali
Bw. Leonard Kushoka, Mkurugenzi wa Kuja na Kushoka Tools Manufacture
Group amesema kuwa kiwanda chake kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 13
na kufanikiwa kubuni teknolojia mbalimbali rafiki kwa mazingira ambapo
mpaka sasa wamefanikiwa kuwafikia vijana zaidi ya 50 katika Wilaya za
Tabora Manispaa, Urambo, Kaliua, Mlele pia Katavi na kufanikiwa
kuwafundisha utengenezaji wa Majiko banifu yanayopunguza matumizi ya
kuni na mkaa kwa asilimia 50.
Pia
Kiwanda hicho kimefanikiwa kubuni mashine ambayo ina uwezo mkubwa wa
kuzalisha kilo 160 kwa saa kwa kutumia dizeli lita 5 na kuzalisha
wastani wa Kilo 1000 za mkaa mbadala na pia Kiwanda hicho kimefanikiwa
kubuni mtambo kwa kukaushia tumbaku kwa kutumia taka kavu au mabaki yote
ya mazao kama maganda ya karanga, randa za mbao, magunzi ya mahindi na
masuke ya mpunga.
Bw.
Kushoka amesema kuwa “Mtambo huu umetoa matokeo mazuri katika ukaushaji
wa tumbaku kwani wastani wa matumizi ya taka kilo 3 hukausha kilo moja
ya tumbaku kwa kutumia mabani ya kisasa”
Bw.
Kushoka amemuomba Waziri kuisaidia Kampuni hiyo kupata mafunzo
mbalimbali ya namna bora zaidi ya kubuni na kuendeleza uzalishaji wa
nishati mbadala hasa katika nchi zinazofanya vizuri zaidi.
‘Kuja na Kushoka” ilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kupata usajili mwaka 2013 na kupewa hati (TMC/CO/CBO/48).
Waziri
Makamba akiwa katika Mkoa wa Tabora pia amepata fursa ya kutembelea
Wilaya ya Nzega na Igunga, akihitimisha ziara yake ya Mikoa 10 hapa
nchini yenye changamoto za kimazingira.


No comments:
Post a Comment